Vienna Fingers

Vienna Fingers ni aina ya biskuti zilizotayarishwa na kampuni ya Keebler, sehemu ya Kellog's. Biskuti hizi huwa zimetayarishwa kwa njia ya safu tatu hasa mbili za nje zalizo ngumu na aina ya siagi ya ladha ya vanila katikati ya hizo mbili za nje. Zikiwa zinafanana sana na kuki za Oreo, biskuti hizi zimechorwa na kuandikwa jina la bidhaa lakini umbo lake ni tofauti hasa kama kidole. Huwa zimepakiwa katika pakiti nyekundu zenye zimeandikwa majina "Vienna Fingers" na rangi nyeupe.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search